23 Agosti 2025 - 23:18
(Radi amali) Mwitikio wa Maduro kwa Kupelekwa kwa Manowari za Marekani Venezuela

Rais wa Venezuela ameikosoa hatua ya Marekani ya kupeleka manowari tatu za kivita karibu na pwani ya nchi yake, akitaja kitendo hicho kuwa ni “uvamizi wa kigaidi wa kijeshi, usio halali na kinyume cha sheria.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-mwanzoni mwa wiki hii, chanzo cha Marekani kilithibitisha kwamba manowari tatu za kivita za aina ya Aegis zilitumwa kuelekea maji ya kimataifa karibu na pwani ya Venezuela, Amerika ya Kusini. Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti pia huenda wanamaji 4,000 wakaambatana na operesheni hiyo.

Nicolás Maduro alilaani hatua hiyo ya Marekani inayodaiwa kufanyika kwa kisingizio cha kupambana na biashara ya mihadarati, na akaieleza kama jaribio “batili la kubadilisha mfumo wa kisiasa wa Venezuela.”

Katika hotuba yake kwa wabunge, Maduro alisema:

Mabadiliko ya utawala ndiyo wanayolitishia taifa letu. Hii ni mashambulizi ya kigaidi ya kijeshi, yasiyo ya kimaadili, ya kihalifu na kinyume cha sheria.”

Akaongeza kuwa suala hili linahusu amani, sheria za kimataifa, Amerika ya Kusini na Karibi, akibainisha kuwa:

“Yeyote atakayeishambulia nchi moja katika Amerika ya Kusini, kiuhalisia anazishambulia nchi zote.”

Ni vyema kukumbuka kuwa mwaka 2020, katika muhula wa kwanza wa urais wa Donald Trump, mahakama ya shirikisho ya Marekani ilifungua mashtaka dhidi ya Maduro na maafisa wengine wakuu wa Venezuela kwa tuhuma za kushiriki katika njama ya “ugaidi wa mihadarati.” Mapema mwezi huu, serikali ya Trump iliongeza maradufu zawadi kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa Maduro kwa tuhuma hizo, na kuifikisha hadi dola milioni 50.

Kwa upande wake, Maduro wiki hii ametangaza kuwa kama sehemu ya majibu kwa vitisho vya Marekani, Serikali yake itawapeleka wanamgambo milioni 4.5 kote nchini Venezuela. Pia ametoa mwito kwa wananchi kufanya maandamano mwishoni mwa wiki kulaani hatua hizo za Washington.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha